WANAHABARI MTWARA WATAKIWA KUELIMISHA JAMII KUHUSU UMUHIMU WA PSSSF

 



Mfuko wa hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kanda ya kusini kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Mtwara (MTPC) wametoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Mtwara kwa ajili ya kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mfuko huo.

 

Mafunzo hayo yametolewa Juni,10, 2025 yakiongozwa na Meneja wa PSSSF kanda ya kusini Bw. Lulyalya Sayi, katika ukumbi Tiffany Diamond hotel mkoani Mtwara.

 


Miongoni mwa mada zilizotolewa katika mafunzo hayo ni pamoja na matumizi ya mfumo wa PSSSF kidigitali unaomwezesha mwanachama kuomba mafao yake kupitia mtandao, kujisajili mwanachama mpya sambamba na kufuatia maendeleo ya akaunti ya mwanachama.

 


“Natoa wito kwa baadhi ya waajiri wanaodaiwa na PSSSF kulipa fedha kwa waajiri wao kwa wakati ili madeni hayo yasikwamishe mafao kwa wanachama na sisi PSSSF ili tuweze kutimiza wajibu wa kuwalipa wanachama kwa wakati.” amesema Sayi.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoa wa Mtwara Grace Kasembe ameishukuru PSSSF kwa mafunzo yaliyotolewa lakini ameahidi kuwa mabalozi wazuri kwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mfuko wa hifadhi ya jamii.

 

Nao baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo hayo wamekiri kupata ujuzi kuhusu mfumo wa hifadhi ya jamii sambamba na kuufanyia kazi katika machapisho mbalimbali katika kuelimisha jamii.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Ramla Masali-Mtwara

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments