Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuchochea maendeleo ya Taifa kwa njia ya ushirikiano wa kimkakati baina ya taasisi zake, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi hususan waishio vijijini.
Katika hatua ya kuimarisha ushirikiano huo, Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) hivi karibuni wamekutana kwa mazungumzo maalum jijini Dodoma, kujadili mikakati ya kujengeana uwezo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkutano huo umejumuisha Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa REA, Martha Chassama; Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TARURA, Catherine Sungura; na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Masoko wa RUWASA, Athumani Shariff.
Aidha, Ushirikiano baina ya taasisi hizo ni chachu muhimu katika kufanikisha maendeleo ya maeneo ya vijijini kupitia huduma za msingi kama umeme, barabara, na maji safi na salama.
Kwa kuunganisha nguvu na kushirikishana uzoefu, taasisi hizo zinaweza kufikia malengo kwa haraka na kwa ufanisi zaidi, hasa katika maeneo yaliyo pembezoni mwa huduma za msingi.
Kikao hicho ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha taasisi za umma zinafanya kazi kwa kushirikiana na kwa ufanisi mkubwa, kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuharakisha maendeleo ya Taifa.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments