Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeitaka jamii kuwa makini na taarifa wanazozisambaza mitandaoni kwa kuhakikisha kuwa ni sahihi na zimethibitishwa kupitia vyanzo rasmi kama vile vyombo vya habari, kurasa za taasisi au kampuni husika.
Katika taarifa yake kupitia mtandao wake wa kijamii wa WhatsApp Channel, TCRA imesisitiza umuhimu wa matumizi ya mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji, ikieleza kuwa kusambaza taarifa zisizohakikiwa kunaweza kusababisha taharuki, upotoshaji na athari kwa jamii nzima.
“Ni wajibu wa kila mtumiaji wa mtandao kuhakikisha taarifa anayoisambaza ni sahihi, imethibitishwa, na haina madhara kwa mtu au jamii,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
TCRA pia imehimiza wananchi kuwa mabalozi wa matumizi salama na sahihi ya teknolojia ya mawasiliano kwa manufaa ya taifa, ikikumbusha kuwa usalama mtandaoni unaanza na mtu binafsi.
Na kudhihirisha kuwa kila mmoja wetu anao mchango mkubwa katika kuhakikisha mitandao inatumika kwa njia chanya. Kwani Usalama Mtandaoni si jukumu la mamlaka peke yake, bali ni jukumu la kila raia.
TCRA imekuwa mstari wa mbele katika kampeni za uhamasishaji kuhusu matumizi salama ya TEHAMA, ikiwa ni pamoja na elimu kwa umma kuhusu athari za kusambaza taarifa za uongo au zisizohakikiwa.#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments