SEKTA YA UTALII NI MHIMILI MUHIMU WA UCHUMI WA TAIFA - DKT. BITEKO

 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko, amesema sekta ya utalii ni mhimili muhimu wa uchumi wa Taifa kwani inachangia asilimia 7.9 ya pato la Taifa na pia ni njia madhubuti ya kuitangaza Tanzania Kimataifa.

 

Hayo ameyasema Juni 06, 2025 alipofungua maonesho ya Karibu Kili-Fair yanayofanyika katika viwanja vya Magereza - Kisongo, jijini Arusha.  

 


Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza programu mbalimbali kama Royal Tour zinazolenga kuimarisha na kutangaza sekta ya utalii duniani kote kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi huku akiipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na waandaaji na washiriki wa maonesho ya Karibu Kili-Fair kwa juhudi zao katika kukuza sekta ya utalii.

 

Aidha, Dkt. Biteko ametoa maelekezo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuandaa mikakati ya kuendeleza mazao ya utalii yenye tija, pamoja na kutumia teknolojia ya TEHAMA katika kuitangaza Tanzania Kimataifa na kusisitiza umuhimu wa kutumia ubunifu na teknolojia ili kuongeza ushindani wa kibiashara kwenye soko la Kimataifa.

 


Vilevile, ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuendelea kuwekeza katika sekta ya utalii huku akiahidi kuwa Serikali itaendelea kuondoa vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya sekta hiyo na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji. 

 

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Paul Makonda, ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kulitambua eneo la Magereza - Kisongo kama eneo maalum kwa ajili ya maonesho ya kimataifa ya utalii ili kuvutia wageni kutoka Mataifa mbalimbali. 

 


Pia ameshauri muda wa maonesho hayo uongezwe kutoka siku 3 hadi siku 5 au 7 ili kutoa fursa zaidi kwa wawekezaji kuonesha bidhaa na huduma zao, hasa zinazohusiana na mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments