Waumini wa dini ya Kiislamu wamekusanyika jijini Dodoma kwa ajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na kuliombea Taifa kwa ujumla, wakisisitiza umuhimu wa kudumisha amani kama msingi wa maendeleo ya nchi.
Akihutubia maelfu ya waumini waliohudhuria mkusanyiko huo uliofanyika Juni 07,2025, katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma, Sheikh Yahya Kivuma kutoka taasisi ya Daarul Arqam ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiombea nchi na viongozi wake, akisisitiza kuwa amani ni nguzo kuu ya ustawi wa Taifa.
"Tunapaswa kuilinda na kuienzi amani tuliyonayo. Mafundisho ya dini yetu yanasisitiza kuwa unapomuombea kiongozi wako, unajibariki mwenyewe, kwani baraka hizo humrudia anayeomba," amesema Sheikh Kivuma.
Sheikh Kivuma amekumbusha pia kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) aliwahi kuomba dua maalum kwa ajili ya mji wa Makkah ili uwe mahali pa amani, akibainisha kuwa hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kufikiwa mahali ambapo amani imekosekana.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi wote, bila kujali tofauti zao za dini au itikadi, kushirikiana kwa pamoja katika kudumisha mshikamano, upendo na utulivu, ili Tanzania iendelee kusonga mbele kwa mafanikio.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments