TANESCO KINARA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeibuka kinara na kukabidhiwa tuzo ya uhifadhi wa mazingira katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa yaliyofanyika  Juni 05, 2025 jijini Dodoma. Ikiwa ni moja ya shirika linaloitendea haki ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, juu ya utunzaji wa mazingira

 

TANESCO imetunukiwa tuzo hiyo kutokana na kutambua mchango katika kuhifadhi mazingira kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ambao umeendelea kuzingatia misingi ya utunzaji wa mazingira sambamba na kuchangia kupunguza gesi joto nchini.

 

Tuzo hiyo ilitolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, katika hafla ya kufunga rasmi maadhimisho hayo.

 

Kwa kuzingatia umuhimu mazingira nchini, TANESCO kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, imedhamiria kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya umeme kwa kuzingatia usalama wa mazingira, ikiwa ni pamoja na JNHPP na mingine inayolenga kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments