Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Madini yanayoendelea katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, yakilenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi na wawekezaji kwenye sekta ya madini. Maonesho hayo yameanza Juni 11 na yanatarajiwa kufungwa Juni 14 2025.
Mgeni rasmi katika kilele hiki cha maonesho haya ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mbunge wa jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa Majaliwa, ambaye amewakilishwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa. Uwakilishi wake ni ishara ya uzito ambao Serikali inaweka katika kukuza uchumi wa madini nchini kupitia ushirikiano wa sekta binafsi na ya umma.
TIC, kama taasisi ya Serikali inayosimamia na kuratibu masuala ya uwekezaji, imetumia jukwaa hilo kuelimisha washiriki kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya madini, ikiwa ni pamoja na usindikaji wa madini, uongezaji thamani, na ujenzi wa viwanda vinavyohusiana na sekta hiyo.
Akizungumza katika banda la TIC, Meneja wa kanda ya mashariki kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Grace Lumunge wa kituo TIC amesema, maonesho hayo ni fursa adhimu kwa wananchi, wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wadau wa maendeleo, kujifunza, kuuliza na kuelewa kwa kina taratibu, faida, na usaidizi unaotolewa na Serikali katika mchakato wa kuwekeza.
TIC pia imetumia maonesho hayo kupokea maoni na maswali kutoka kwa washiriki, jambo linalosaidia katika kuboresha huduma zake na kufanikisha dhamira ya Serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda unaotegemea rasilimali za ndani, ikiwemo madini.
Kwa kushiriki maonesho haya, TIC imeonesha kwa vitendo namna taasisi za umma zinavyopaswa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya Taifa kwa kushirikiana na wananchi na sekta binafsi.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments