Wananchi wa mkoa wa Lindi wamemhakikishia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kura zote za ushindi zitaanzia mkoa wa Lindi, ushindi ni wa CCM sambamba na Wabunge na Madiwani wa CCM mkoani humo. Wameahidi pia kutimiza wajibu wao wa kutiki ifikapo Oktoba 2025.
Hayo yamejiri Juni 14, 2025 katika Kilele cha Maonesho ya Madini katika Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, ambapo Mgeni Rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Kassim Majaliwa Majaliwa, ambaye amewakilishwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa.
Aidha, Kauli Mbiu ya Maonesho hayo ni: Madini na Uwekezaji fursa za kiuchumi Lindi, Shiriki Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2025 ambapo Mkuu wa mkoa Lindi Hajjat Zainab Telack amesema,
"Serikali inaagiza uwekezaji katika madini ili iweze kupata mrabaha, sambamba na kusisitiza wajibu wa kulipa kodi kwa wachimbaji na wawekezaji ili kuweza kuchangia jitihada za maendeleo nchini." Amesema Hajjat Telack.
Pia ametoa rai kwa Watanzania wote kuwekeza katika sekta ya madini ili kuweza kukuza uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla.
Sambamba na hayo, Amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumuamini na kumkabidhi mkoa wa Lindi ambao umekuwa darasa kwake na kwa wenzake pia, amemuahidi kuendelea kupambana kwa kushirikiana na viongozi wenzake, ili kuhakikisha wanaongoza wananchi kuwekeza katika maeneo yote ambayo yana fursa, kama kauli mbiu ya mkoa huo inavyosema, Kimbilia Lindi, kimbilia fursa
Naye Mgeni Rasmi wa maadhimisho hayo Dkt. Kiruswa amewapongeza viongozi na wananchi wa mkoa wa Lindi kwa kufanikisha maonesho hayo yaliyofana, pia amewasilisha salam za Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusema,
"Mheshimiwa Waziri Mkuu amenituma niwasisitizie kulinda amani, mshikamano na kushiriki zoezi la Kitaifa la Uchaguzi Mkuu Octoba 2025.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments