TIC YASHIRIKI WIKI YA MADINI NCHINI DRC

 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Benki ya CRDB kinashiriki Wiki ya Madini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC Mining Week) ambayo imeanza tarehe 11 Juni na kuhitimishwa 13 Juni 2025 katika mji wa Lubumbashi. 

 

Maonesho na Mikutano huu ni miongoni mwa Mikutano mikubwa barani Afrika katika uwekezaji kwenye sekta hii ya madini. Zaidi ya washiriki 10,300 kutoka sekta hii wameshiriki kutoka ndani na nje ya DRC. Kwa kutumia mikutano na Maonesho ya mwaka huu ya Wiki ya Madini Kituo cha Uwekezaji kimeweza kuvutia na kuhamasisha uwekezaji hususan katika sekta za madini, nishati safi, kilimo na usafiri na usafirishaji. 

 

Katika hatua nyingine TIC na CRDB wameweza kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mdogo wa Tanzania katika mji wa Lubumbashi (Consul General), Magabilo Innocent Murobi ambaye amepongeza hatua ya taasisi hizo na TPA kushiriki katika tukio hili kubwa barani Afrika katika sekta za kiuchumi na kutoa rai kwa taasisi nyingine kutoka Tanzania kuiga mfano huo.

 

Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimewakilishwa na Meneja wa Uhamasishaji wa Nje, Daudi Riganda.

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments