SIMBA NA YANGA WAKUTANA NA RAIS SAMIA IKULU, DODOMA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Juni 13, 2025, ametenga muda maalum kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa klabu mbili kongwe na zenye ushindani mkubwa nchini Klabu ya Simba na Klabu ya Yanga, katika kikao kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.

 

Katika mtandao wake wa kijamii Rais Samia amendika;

"Ijumaa ya kazi ofisini Ikulu, Chamwino, Dodoma ambapo pia nilitenga wasaa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Klabu ya Simba na wa Klabu ya Yanga".

 


Aidha, kikao hicho kimefanyika katika kipindi ambacho mashabiki na wadau wa soka nchini wamekuwa wakijadili kwa hisia kali sintofahamu iliyoibuka kati ya klabu hizo mbili, kuhusu timu zote mbili kususia darby  pamoja na malalamiko mbalimbali kuhusu haki na usawa kwenye uendeshaji wa mashindano.

 

Rais Samia amekutana na viongozi wa pande zote mbili kwa lengo la kusikiliza hoja zao, kuhimiza mshikamano, na kuhimiza umuhimu wa kulinda amani na taswira ya michezo nchini, hasa ikizingatiwa kuwa soka ni mchezo unaowaunganisha Watanzania wengi na kuwa chanzo cha ajira, burudani, na mshikamano wa Kitaifa.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais kukutana na pande hizi mbili kwa wakati mmoja tangu mvutano wa hivi karibuni ulipojitokeza. Hata hivyo, hatua hii ya Rais inatafsiriwa na wengi kama jitihada za kulinda heshima ya michezo nchini na kuzuia mivutano isiyokuwa na tija.

 

Kwa sasa, wadau wa soka wana matumaini ya kuziona timu zao hizo zikiingia ndimbani hivi karibu, kwa kuwa busara imetumika, kikao cha Ikulu kimetoa mwelekeo mpya wa maelewano kati ya klabu hizi kongwe.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv


Post a Comment

0 Comments