WANAWAKE MANISPAA YA MTWARA WAKOPESHWA MIL 375.5

 

Manispaa ya Mtwara-Mikindani imekabidhi mkopo usio na riba wa zaidi ya Sh. Mil 375.5 kwa vikundi 59 vya Wanawake, ikiwa ni fedha kutoka kwenye mfuko wa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.

 

Kiasi hicho kilichokabidhiwa awamu ya Pili kinafanya Manispaa hiyo kukabidhi zaidi ya Sh. Bil 1.016 katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.

 

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mkopo huo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Shadida Ndile amewataka wanawake hao kutumia fedha walizokopeshwa kuendeleza mitaji yao ili waweze kurejesha mkopo kwa wakati na vikundi vingine viweze kukopeshwa na kufaidika na mkopo huo.

 

“Sitegemei kuona hapo baadae tutakuja kukamatana, kunyang’anyana vitu na kupelekena polisi, ninaamini fedha hizi zitaenda kuinua mitaji yetu ili fedha zirudi na turejeshe mikopo yetu ili na wengine wakope tena” Ndile.

 

Amesema kuwa Manispaa haina ubaguzi kwenye utoaji wa mikopo kwa kuwa inazingatia kanuni, sheria na miongozo iliyowekwa, hivyo amewataka wanawake hao kuwa mabalozi kwa watu wengine ambao hawakufanikiwa kupata mikopo kwa awamu hii ili kuondoa dhana ya uwepo wa upendeleo kwenye zoezi hilo.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi. Juliana Manyama amewasisitiza wanawake hao kuwa wavumilivu na kuepuka kutumia lugha za matusi na kejeli kwa viongozi na Maafisa wanaohusika na mikopo pindi mchakato wa mikopo unapokuwa unaendelea kwa kuwa wahitaji ni wengi na fedha za ukopeshaji zinategemea na urejeshaji wa mikopo ya vikundi.

 

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wenzake Jesca Masanja mkazi wa majengo amesema kuwa, wanatarajia mkopo huo utawanufaisha kiuchumi na kutoa wito kwa wanawake wengine kuchangamkia fursa pale mikopo inapotangazwa .

 

Mwezi Januari mwaka huu, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ilikopesha mkopo usio na riba zaidi ya shilingi Mil. 640.9 kwa vikundi 58 vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mtwara

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments