DC MBEYA AZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA 5 JIJI LA MBEYA

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amezindua mpango mkakati wa Dira ya Maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ambayo italeta tija na mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali.

 

Mkakati huo umetajwa kugusa mambo zaidi ya 29, ikiwemo sekta ya elimu, afya, mikopo asilimia 10 ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kuboresha mifumo ya Tehama, ujenzi wa Bandari kavu ambayo itachochea uchumi.

 

Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa mkapa jijini hapa ,huku Mkuu huyo wa Wilaya Beno Malisa akisisiza ukawe chachu ya kubadilisha Jiji la Mbeya hususani ujenzi wa kituo cha watoto yatima kije na suruhisho la kupatiwa elimu ya kujiajiri.

 

Malisa amesema hayo mara baada ya Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ,Abdallah Nnunduma kuwasilisha mpango mkakati huo kwa wananchi wakiwepo watendaji wa serikali na madiwani

 

"Nimeona mpango mkakati wa mwaka 2029 mkapa 2039 ,ukienda kutekelezwa vizuri utakuwa na tija kubwa hususani kutupia jicho kwa kundi la watoto mazingira magumu"amesema.

 

Meya wa Jiji la Mbeya,Dourmohamed Issa amesema mkakati huo unakwenda kuleta chachu ya kubadili taswira ya Jiji na kusisitiza suala la lishe  bora ambalo ipo kwenye mpango huo litiliwe mkazo.

 

Amesema  katika mchakato wa kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano baraza la madiwani limeshiriki kikamilifu .

 

Mkazi wa Mabatini Lucy Zakalia ,amesema mpango huo umetaja mambo mbalimbali ikiwepo uwekezaji kwenye sekta ya elimu,afya ,ujenzi kituo watoto yatima sambamba na ujenzi wa bandari wa nchi kavu.

 

Amesema wana kila sababu ya kuipongeza halmashauri kwa kuja na mkakati huo ambao utakuwa chachu katika kuleta maendeleo kwa jamii

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments