Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ameridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa mradi mkubwa wa kimkakati kutoka chanzo cha Mto Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Waziri huyo ametoa kauli hiyo jana Jumatano Julai 23,2025 mara baada ya kufanya ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa mradi huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya (Mbeya Uwsa)na kujengwa na mkandarasi wa kampuni ya China Rarway Construction Engineering Group chini ya Mhandisi mshauri GkW Consult GmbH.
Amesema ameridhishwa na hatua ya utekelezaji wake huku akimtaka mkandarasi kuongeza nguvu ya usambazaji wa mabomba na nguvu kazi.
"Niwape pongezi kubwa Mkuu wa Mkoa,Bodi ya Maji Mbeya Uwsa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mradi huu mkubwa wa kimkakati, "amesema.
Pia Waziri Aweso amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Beno Malisa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji ukiwepo wa miji 28 Wilaya ya Mbarali na kuchukua hatua kwa watakao kwamisha.
Aweso pia katika ziara yake ametembelea mradi wa miji 28 katika eneo la Rujewa Wilaya ya Mbarali utakao gharimu sh 130 bilioni kutokana na fedha za ufadhiri wa Serikali ya India.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Beno Malisa amemuomba Waziri Aweso kuona namna ya kuboresha miradi 15 inayotekelezwa na Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) ili kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya (Mbeya -Uwsa )CPA Gilbert Kayange amesema mradi wa chanzo mto Kiwira umefikia asilimia 45 utakamilika Desemba mwaka huu
Amesema mradi huo utagharimu zaidi ya Sh bilioni 119 na kuzalisha lita 117 milioni kwa siku na kupelekea ongezeko la upatikanaji wa huduma kwa wananchi wa Mji wa Mbalizi na Mkoa wa Mbeya.
Mkazi wa Kiwira Subira Mwakyusa amesema hiyo ni fursa kwao katika kuondokana na hadha iliyopo katika baadhi ya maeneo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments