ATAKAENG'OA KITI UWANJA WA MKAPA KUKIONA

 

Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa inatarajia kufunga Kamera zaidi ya 200 kwenye uwanja wa Mkapa na mtu yeyote atakaevunja kiti au kifaa chochote uwanjani hapo atashughulikiwa binafsi.

 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Desemba 18,2024 kwenye Mkutano wa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi na wadau wa sekta ya Habari na Utangazaji, unaofanyika jijini Dar es Salaam.

 

Msigwa amesema, baada ya ukarabati wa uwanja huo kukamilika hakutakuwa na huruma kwa mtu yeyote atakaeng'oa viti au kifaa chochote cha uwanja huo.

 

"Ndugu zangu naomba niwaambie, tunakwenda kufunga kamera zaidi ya 200 kwenye uwanja wa Mkapa, yeyote atakaeng'oa kiti au kifaa chochote kile, tutashughulika nae yeye binafsi, hayo ya faini kwa klabu yatabaki kwa TFF na CAF.

 

"Kwa hiyo ujumbe uwafikie wote wenye tabia ya kung'oa viti, tutadili na mtu binafsi," amesema Msigwa.

 

Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments