MAONESHO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KIBAHA SASA KUWA YA KITAIFA

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeagiza Maonesho ya Biashara na Uwekezaji, yaliyozinduliwa Disemba 17,2024 Kibaha Mkoa wa Pwani, kuanzia mwaka 2025, yapandishwe hadhi ya kuwa maonesho ya Kitaifa na kusimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Mkoa wa Pwani.

 

Akitoa maagizo hayo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Waziri wa Viwanda Dkt.Selemani Jafo amesema kuwa, kutokana na maonesho hayo kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, yanastahili kupandishwa hadhi na kusimamiwa na Wizara hiyo.

 

“Kuanzia sasa maonesho haya ya Biashara na Uwekezaji yawe maonyesho ya Kitaifa na yasimamiwe na Wizara ya Viwanda na Biashara kushirikiana na Mkoa wa Pwani, na kwamba kila mwaka yafanyike ndani ya Mkoa wa Pwani, lazima tusonge mbele, Watu wakifanya vizuri tuwasifie tusingoje wafe, RC Pwani na Viongozi wako mnafanya vizuri endeleeni kuchapa kazi,” amesisitiza Waziri Dkt.Jafo.

 

Waziri Dkt. Jafo amewapongeza viongozi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani, kwa maandalizi mazuri ya maonesho hayo.

 

Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments