BREAKING NEWS: SELEMANI SANKWA AFARIKI DUNIA


 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Selemani Sankwa, amefariki dunia leo Desemba 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam, alikokua akipatiwa matibabu.

Sankwa ambaye ameugua kwa kipindi kifupi aliwahi kulazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma, akapata matibabu kisha kuruhusiwa na kuendelea na shughuli zake licha ya kutokuwa katika utimamu nzuri wa afya yake.

Baadae alitekeleza majukumu yake kama katibu wa CCM Mkoa wa Tanga kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo baadae hali yake ikabadilika na kupelekea kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuanza kupata matibabu.

Baada ya uchunguzi zaidi ikabainika kuwa na matatizo ya Moyo ndipo akahamishiwa JKCI ambako umauti umemfika akiwa katika taasisi hiyo ya Moyo akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Tandahimba Katani Ahmed Katani, ni kwamba mwili wa Samkwa unatarajiwa kusafirishwa hadi mkoani Mtwara kesho Desemba 21 huku mazishi yakitarajiwa kufanyika Jumapili Desemba 22, 2024 saa 4 asubuhi.

 

#TanguliaSankwaSoteNjiaNiMoja

 

 

#KhomeinTvUpdates 

 

Juma Mohamed

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments