AJALI YA BASI YAUA WANAFUNZI 5 NA KUJERUHI 9 CHUNYA

 

Wanafunzi  watano wa Shule ya Sekondari Chalangwa Wilaya ya Chunya,wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya kugongwa na basi la abiria mali ya kampuni ya Safina Coach linalofanya safari kutoka Wilaya ya  Chunya  kwenda  Mbeya mjini.

 


Ajali hiyo imetolea leo Julai 26 mwaka huu majira ya saa 11.30 alfajiri katika kijiji cha Itumba  Kata ya Chalangwa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya wakati wanafunzi  hao wakikimbia  mazoezi ya mchaka mchaka .

 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa amewataja walio poteza maisha kuwa ni Seleman Ernest,  Samweli Zambi, Kelvin Mwasamba,Hosea Mbwilo, na Amina Ulaya 

 


Aidha ametaja majeruhi saba kati ya tisa waliolazwa katika Hosptali  ya Wilaya ya Chunya na Kituo  cha Afya Chalangwa  kuwa ni , Bernard Mashaka (17), Lilian Raymond (16), Kennedy Masoud (14),Vicent Malema(17),Siwema Nasib (17),Alex Peter(17),Dethani Charles(15), na wengine wawili  Getruda Mwakyoma (17), na Farida Mwasongole (17),wametibiwa na kuruhusiwa.

 

Ameasema ajali hiyo  ilihusisha basi la kampuni  ya  Safina Coach Kenya namba za usajili   T 194 DCE lililokuwa likitokea Chunya mjini kuelekea Mbeya likiendeshwa na Dereva Abdul Hassan (28),Mkazi wa jijini hapa.

 

 

Amesema chanzo cha ajali ni dereva wa gari hilo  kushindwa  kulimudu na kisha kuwagonga wanafunzi hao na kusababisha vifo na majeruhi.

 

Imeelezwa dereva wa baai hilo baada ya kusababisha ajali hiyo ametoweka na kwamba  Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments