Miili ya wanafunzi Sita waligongwa na basi la kampuni ya Safina Coach, imeagwa Jumapili Julai 27 mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Msingi Chalagwa iliyopo Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.
Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa chama na serikali wameshiriki wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mbarak Batenga.
Wadau wengine ni pamoja na Mfanyabiashara wa Madini Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya, Geofrey Mwankenja ambaye ametoa ubani wa Sh 5.5 milioni kwa familia za wanafunzi waliopoteza maisha baada ya kugongwa na basi hilo.
Ibada hiyo pia imehudhuriwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Kasaka.
Ajali hiyo ilitokea Julai 26 majira ya saa 11.30 alfajiri wakati wakikimbia mchaka mchaka katika kijiji cha Itumba Kata ya Chalangwa Wilayani humo na kusababisha vifo vya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chalangwa Sita na tisa kujeruhiwa.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments