DOLA BIL. 248 KUSAIDIA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WANAWAKE TANZANIA

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Benki ya Dunia, wamesaini mikataba miwili yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 104 sawa na takribani Shilingi Bilioni 248 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania, maarufu kama “PAMOJA”.

 

Msaada huu ni jitihada za Rais wa awamu ya Sita, Dkt. Samia katika kuhakikisha wanawake wanapata fursa za kiuchumi pamoja na huduma za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia Tanzania Bara na Zanzibar. 

 


Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika Jijini Dar es Salaam Disemba 12, 2024 kati ya Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba, kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete. 

 

Mikataba hiyo imejumuisha mkataba wa Dola za Marekani Milioni 4 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 9.5 ni za msaada na Mkataba wa Dola za Marekani Milioni 100 sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 238 ni mkopo wenye masharti nafuu.

 

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema, mradi wa PAMOJA utasaidia kuongeza upatikanaji wa fursa za kiuchumi kwa wanawake pamoja na huduma za kuzuia na kukabiliana na ukatili wa kijinsia Tanzania Bara na Zanzibar. 

 


Amesema hilo litatimizwa kupitia uimarishaji vikundi vya wanawake kwa kuwajengea ujuzi wa biashara na kuwaunganisha na fursa za masoko, kuongeza fursa za mikopo nafuu kwa vikundi vya wanawake, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wanawake kupitia mifumo rasmi ya kifedha na kuimarisha huduma za kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

 

"Hili litatimizwa kupitia uimarishaji vikundi vya wanawake kwa kuwajengea ujuzi wa biashara na kuwaunganisha na fursa za masoko, kuongeza fursa za mikopo nafuu kwa vikundi vya wanawake, kuwaongezea upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia mifumo rasmi ya kifedha pamoja na kuimarisha huduma za kukabiliana na ukatili wa kijinsia”, amefafanua Dkt. Nchemba.

 

Amesema mradi huo utawanufaisha moja kwa moja wanawake wapatao 319,850 na walengwa wengine 399,000, wakiwemo wanafamilia za wanufaika.

 

Amesistiza kuwa kukuza usawa wa kijinsia si suala la wanawake pekee bali ni msingi wa Taifa la kidemokrasia, lenye haki na linalostawi na kuongeza kuwa kuondoa tofauti za kijinsia kunaboresha uzalishaji na kuimarisha uhimilivu wa kiuchumi.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments