SERIKALI YAIMARISHA THAMANI YA SHILINGI MBELE YA DOLA YA MAREKANI

 

Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya mambo makubwa, ambapo sasa imeweza kuongeza uwezo wa kuuza bidhaa zake nje ya nchi hatua inayotajwa kusaidia kuongeza fedha za kigeni na kuimarisha thamani ya shilingi mbele ya dola ya Marekani.

 

Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, thamani ya Dola ya Marekani imepungua katika soko la fedha la kimataifa kiasi cha kuzua mjadala miongoni mwa wataalam wa masuala ya uchumi na fedha, huku baadhi wakitaja kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi kama kichocheo cha kuimarika kwa shilingi ya Tanzania.

 

Utafiti unaonyesha bidhaa za kilimo kama korosho na parachichi, pamoja na mauzo ya dhahabu, vimechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato ya fedha za kigeni.

 

Ripoti kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonyesha kuwa katika mwaka ulioishia Julai 2024, Tanzania ilikusanya shilingi trilioni 34 kutoka kwa mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi, ongezeko ambalo limeimarisha uthabiti wa shilingi dhidi ya dola ya Marekani.

 

Pia inaonyesha sekta ya utalii, ambayo ni mojawapo ya nguzo kuu za uchumi wa Tanzania, nayo imeonyesha ukuaji wa kasi.

 

“Kwa mujibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024 pekee, Tanzania ilivutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) wenye thamani ya dola bilioni moja za Marekani ikiwa ni ongezeko la asilimia 53 ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana.” 

 

 Sababu nyingine zilizochangia hatua hiyo ni mikakati thabiti ya kifedha inayotekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesaidia kudhibiti mfumuko wa bei, ambao umekuwa katika kiwango cha asilimia 3-5, kiwango kinachokubalika kimataifa kwa uchumi imara.

 

“Kupitia usimamizi makini wa mzunguko wa fedha, BoT imehakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa na mazingira mazuri ya kiuchumi kwa wawekezaji wa ndani na nje. Hii imesaidia kuongeza imani ya wawekezaji na kuimarisha zaidi thamani ya shilingi.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments