SERIKALI YA RAIS SAMIA YATILIA MKAZO KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI


 Katika kujali Afya na usalama wa mazingira na wananchi wake, Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kusimamia utekelezaji wa katazo la kisheria la matumizi ya mifuko ya plastiki, usimamizi wa biashara ya kaboni ili kuongeza msukumo wa Sekta ya hifadhi ya mazingira nchini, na hii kwa faida ya afya ya binadamu, wanyama na mazingira.

 

 Madhara ya mifuko ya plastiki. 

 

Ikumbukwe kuwa, Mifuko ya plastiki ni aina ya mifuko yenye mchanganyiko wa kemikali zisizooza hivyo kuleta athari kwenye mazingira pamoja na afya kwa binadamu na Wanyama.

 

Inakadiriwa kuwa, matumizi ya mifuko ya plastiki Duniani ni Bilioni 500 mpaka Trilioni moja nchini Tanzania ambapo tani 350,000 ya mifuko ya plastiki huzalishwa kila mwaka, hii ni chini ya asilimia kumi (10%) ya mifuko iliyotumika hurejereshwa. 

 

Kutokana na tafiti mbalimbali mifuko ya plastiki huchukua miaka 400 mpaka 1,000 kuoza ardhini na kusababisha athari mbalimbali  ikiwemo, kuathiri mifumo Ikolojia ya Bahari, ambapo inakadiriwa viumbe Bahari 100,000 na Ndege Bahari Millioni moja hufa kila mwaka kwa kula mifuko ya plastiki.

 


Kuchafua Miji kutokana na kushindwa kuoza na kuathiri mifugo ambapo Ranchi ya Kongwa Mkoa wa Dodoma Ng’ombe 57 walikufa mwaka 2017 kutokana na kula mifuko ya plastiki.

 

Athari nyingine zimetajwa kuwa, ni kuharibu miundombinu kwa kuziba kwenye mifereji na baadhi ya njia za maji, kubeba na kusambaza viumbe vamizi na bacteria, inapochomwa moshi wake una madhara (Casinogenic Compounds) na unaweza kusababisha maradhi ya Saratani.

 

Kutokana na madhara ya mifuko ya plastiki, Serikali ilitoa tamko la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki 1 Juni, 2019 na kuandaa Kanuni ya Usimamizi wa katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki iliyotoka kwenye Gazeti la Serikali.

 

Kwa mujibu wa Kanuni, ni marufuku kutengeneza, kuuza, kusafirisha ndani na nje ya nchi, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote, lengo la Serikali kutengeza kanuni hiyo ni kutokana na athari mbalimbali zitokanazo na mifuko.

 

Muitikio wa utekelezaji wa sheria hii ni pamoja na matumizi ya mifuko mbadala kwa ajili ya kubebea bidhaa. 

 

Mnamo Disemba 13, 2024 wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi baina ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yusuf Masauni na aliyekuwa Waziri wa Ofisi hiyo, Dkt. Ashatu Kijaji aliyehamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Masauni ameahidi kusimamia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.

 

Masauni amesema, mwaka 2019 Serikali ilitoa maelekezo mahsusi kuhusu katazo la mifuko ya plastiki na kusema Ofisi hiyo itaongeza kasi ya usimamizi wa katazo hilo ili kulinda afya ya jamii, Wanyama na mazingira.

 

“Tutashirikiana na Menejimenti ili kuhakikisha tunaongeza kasi katika kusimamia masuala ya katazo la mifuko ya plastiki, usimamizi wa biashara ya kaboni na utoaji wa vyeti vya tathimini ya mazingira (EIA) ili kufikia malengo tuliyojiwekea” amesema Waziri Masauni.

 

Kwa upande mwingine Waziri Masauni ameahidi kushirikiana na Menejimenti na watumishi wa ngazi zote ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo katika kuwahudumia wadau mbalimbali kupitia sekta za Muungano na Hifadhi ya Mazingira nchini.

 

Katika kufanikisha hilo, kwa ufadhili wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), NEMC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inafanya tafiti ya ‘Study of Non-Woven Carrier Bags Manufactured and/or marketed in Tanzania to Determine the Physical and Chemical Characteristics'.

 

Wadau wengine katika utafiti huu ni pamoja na Kitivo cha Kemia na Kitivo Cha Uhandisi wa Madawa na Usindikaji, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Taasisi ya Tafiti na Maendeleo kwa Viwanda (TIRDO), na Shirika la Viwango la Taifa (TBS), ambapo wataalam kadhaa kutoka taasisi hizo wameainishwa kwa ajili ya zoezi zima la utafiti wa sifa za mifuko mbadala (Non-Woven) inayotumika kwa sasa.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments