Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea na mkakati wake wa kuhakikisha Wananchi wake wanapata huduma zote muhimu, kwa ajili ya maendeleo yao, kwa kufanya tathmini kuona maeneo yenye changamoto na yale ambayo bado hayajafikiwa ili kuongeza kipaumbele kwenye nusu ya pili au katika bajeti inayofuata ya mwaka 2025/2026.
Katika kufanikisha azma hiyo, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amezielekeza Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya tathmini ya utekelezaji ya mpango wa bajeti kwa nusu mwaka.
Mhandisi Mativila ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2025/2026 kwa Wataalamu toka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi za Wakuu wa Mikoa Mamlaka za Serikali za Mitaa kinachofanyika Jijini Dodoma.
“Hakikisheni mnafanya tathmini ya nusu mwaka ya utekelezaji wa mpango wa bajeti ili kujiridhisha na hali halisi ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/2025,” Mhandisi Mativila.
Lengo la Tathmini hii ni kuona maeneo yenye changamoto na yale ambayo bado hayajafikiwa ili kuongeza kipaumbele kwenye nusu ya pili au katika bajeti inayofuata ya mwaka 2025/2026.
Mhandisi Mativila amezielekeza Ofisi za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kwenda kusimamia utekelezaji wa maagizo ya Kamati za kudumu za Bunge.
“Kuna maelekezo na maagizo yalitolewa na Kamati za kudumu za Bunge za TAMISEMI, LAAC na PAC hivyo mkasimamie utekelezaji wake na kuwasilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI ifikapo mwezi Februari mwaka 2025 kwa ajili ya kujiridhisha na utekelezaji wa maagizo hayo,” amesema.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments