Dhamira kuu ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kuandaa michuano ya AFCON mwaka 2027, lakini pia ni kuhakikisha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inavunja rekodi kwenye fainali hizo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema Serikali itashirikiana na wadau ili kuiandaa Taifa Stars kuvunja rekodi ya kutokuvuka hatua za awali za michuano hiyo ambayo itaandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Uganda na Kenya.
Mwinjuma ameyasema hayo Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, alipokuwa akifungua Mkutano wa 19 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambapo amewataka wadau kuungana pamoja kwenye maandalizi ya timu ya Taifa ya miguu hasa inapokwenda kushiriki mashindano ya Afrika kama wenyeji ili kipindi hiki kiwe ni cha kuweka historia kwani itakuwa ajabu mwenyeji kutolewa hatua za awali.
“Tunapokwenda kuandaa CHAN na AFCON kuna ushiriki wetu wa aina mbili, wa kwanza ushiriki kama waandaaji ambapo kwa sehemu kubwa Serikali inafanya jukumu lake la kujenga miundombinu na kuhakikisha kila kinachohitajika kinafikiwa na hakuna mahali tunakwama, la pili ushiriki wetu kama washiriki tunaokwenda kucheza, litakuwa jambo la ajabu tunaandaa AFCON halafu tukawa watu wa kwanza kutolewa.”
“Tunashiriki AFCON lakini hatujawahi kuvuka raundi ya awali, mimi kwa nafasi niliyonayo kwa kushirikiana na ninyi TFF na wajumbe wa mkutano huu ambao mnaoendesha mpira wa miguu kote nchini moja ya malengo yangu makubwa ni kuhakikisha tunavunja rekodi hii hatuishii tena raundi ya kwanza.”
Amewapongeza Wajumbe wa Mkutano Mkuu chini ya rais wa TFF, Wallace Karia kwa mafanikio makubwa ambayo yamepatikana mwaka huu kwa timu za Taifa (Taifa Stars) kufuzu AFCON 2025, Twiga Stars kwa kufuzu WAFCON 2025, timu ya U20 (Ngorongoro Heroes) kwa kufuzu AFCON ya U20, na timu ya wavulana ya U15 kuibuka mabingwa wa michuano ya shule ya Afrika chini ya CAF ambayo fainali zake zilifanyika Mei 2024 kisiwani Zanzibar.
Mwinjuma ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na TFF kuhakikisha timu za Taifa pamoja na klabu zinafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Mkutano huo wa kila mwaka umewakutanisha wajumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments