POLISI MBEYA WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA SIKUKU ZA MWISHO WA MWAKA

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewaonya wananchi kuepukana na matumizi ya pombe kupita kiasi wanapo sherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka katika maeneo ya fukwe za ziwa Nyasa.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema hayo leo jumanne Desemba 24,2024 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na namna Jeshi hilo walivyojipanga kuimarisha ulinzi.

 


Amesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha watanzania wana sherehekea sikukuu ya Krismass na Mwaka Mpya kwa amani na utilivu sambamba na kuimarisha ulinzi katika maeneo ya nyumba za ibada.

 


"Tutafanya Doria maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya, sambamba na kupiga marufuku upigaji wa milipuko ya fataki na disco toto maeneo yasiyo ya wazi ili kulinda sheria ya mtoto sambamba na kuonya wamiliki wa kumbi za starehe,"amesema.

 


Pia, Kuzaga amesema ametoa maelekezo kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa vyombo vya moto na kuwapima kiwango cha ulevi madereva lengo ni kudhibiti ajali zisizo za lazima.

 

"Tumeweka mikakati kila dereva atakaguliwa kilevi kwa kipimo maalum kwa watakaobainika watafungiwa leseni kwa muda usio julikana"amesema.

 


 Kuzaga ameongoza doria ya utayari kwa askari wa Jeshi hilo ikiwa ni maandalizi ya kuimarisha ulinzi katika sikukuu za mwisho wa mwaka na kutoa wito kwa wazazi kuwa walinzi wa watoto ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments