SERIKALI KUREJESHEA MADINI YA WAFANYABIASHARA

 

Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan imeahidi kuwarejeshea Madini, wahusika wote, yaliyochukuliwa katika mnada wa mwisho uliofanyika mwaka 2017 na kupelekwa Benki Kuu ili waendelee kufanya biashara.

 

Maamuzi hayo yametolewa kufuatia Serikali ya awamu ya Sita kuona umuhimu wa Wafanyabiashara hao kuendelea kuuza madini yao, na hii ni hatua kubwa ya Serikali katika kujali na kuthamini Sekta ya Madini na Uwekezaji nchini.

 

Katika kutoa taarifa hiyo, Waziri wa Madini, Antony Mavunde amewahakikishia Wauzaji wa madini walioshiriki katika mnada wa madini Mirerani kuwa, Serikali haitochukua madini yao yatakayobaki baada ya kumalizika kwa mnada huo na kuwataka kufanya biashara kwa kujiamini.

 

Mavunde ameyasema hayo wakati akizindua mnada wa madini katika Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Arusha mbele ya Wafanyabiasha mbalimbali wa madini waliojitokeza kushiriki katika mnada wa madini katika eneo hilo.

 

Waziri Mavunde ameongeza kuwa, madini hayo yaliyochukuliwa katika mnada huo wa mwisho uliofanyika mwaka 2017 na kupelekwa Benki Kuu hayajapotea na kwamba yamehifadhiwa kwa usalama na tayari yameshatolewa na Wahusika watarudishiwa ili waendelee kufanya biashara ya madini yao.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments