SERIKALI YAFANIKISHA KULETA MABEHEWA 264 YA SGR KUTOKA CHINA

 

Serikali ya awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikisha kuleta nchini Mabehewa 264 ya mizigo, yatakayotumika katika Reli ya Kiwango cha Kimataifa SGR, ambayo yamewasili kupitia Bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini China, Disemba 24,2024.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania, Fredy Mwanjala, zimeeleza kuwa, zoezi la ushushaji mabehewa hayo kutoka kwenye Meli litakapokamilika, litafuatia zoezi la majaribio, ambalo litajikita katika kutembeza Mabehewa hayo, kwenye Reli yakiwa tupu na kisha yakiwa yamebeba mizigo.

 

Mabehewa hayo yatakuwa yakitembea kwa kasi ya Kilometa 120 kwa saa.

 

Majaribio yatakamilika mara tu Wataalamu wa Shirika la Reli na wale Wakandarasi watakaporidhika kuwa, utendaji kazi wa Mabehewa hayo, umekidhi viwango kulingana na Mkataba rasmi wa kuanza oparesheni za Mabehewa hayo, Shirika litaujulisha Umma.

 

Katika mabehewa 264 yaliyowasili nchini, mabehewa 200 ni ya kubeba makasha (Makontena) na Mabehewa 64 ni ya kubeba mizigo isiyofungwa (Loose Cargoes).

 

Shehena hiyo ya Mabehewa 264 ni sehemu ya jumla ya Mabehewa 1,430 ambayo kwa mujibu wa mkataba, yanatengenezwa na Kampuni ya CRRC ya nchini China.

 

Awali Novemba 15, 2024 Shirika liliutaarifu Umma kuwa, utengenezaji wa Mabehewa 264 ya mizigo, yatakayotumika katika Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR), umekamilika nchini China na Meli iliyobeba mabehewa hayo iling'oa nanga katika Bandari ya Dalian nchini China, Novemba 12,2024.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments