Serikali kupitia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hivi karibuni imefanya vipimo na kutoa chanjo ya Homa ya Ini kwa watoa huduma za afya 100 wa Kitengo cha dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili na wanafunzi 500 wa Chuo cha Sayansi Muhimbili (MUHAS).
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Mohamed Janabi, amesema kuwa, Muhimbili kwa Kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wamezindua mpango wa kuwapatia chanjo dhidi ya Virusi vinavyosababisha Homa ya Ini (Hepatitis B Vaccine) kwa wafanyakazi hao na wanafunzi Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili (MUHAS).
“Leo nimeshiriki uzinduzi wa zoezi la upimaji na chanjo ya homa ya Ini kwa watoa huduma za afya kitengo cha dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili na wanafunzi wa Chuo cha Sayansi Muhimbili,” amesema Prof. Janabi.
Amefafanua kuwa, chanjo hii ni muhimu sana kwa watoa huduma za afya ambao wako kwenye hatari mara 10 zaidi ya kupata maambukizi ya Homa ya Ini ikilinganishwa na watu wa kawaida.
Kwa mujibu wa WHO, mwaka 2022, zaidi ya watu Milioni 254 walikuwa wakiishi na maambukizi sugu ya Homa ya Ini, na zaidi ya watu Milioni 1 walifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana nayo kama saratani ya ini.
Aidha Dkt. Janabi amewasihi wananchi kuchukua hatua sasa ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kupata chanjo, ambayo ni salama, bora, na rahisi kupatikana.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments