WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO WATAKIWA KUCHANGAMKIA MABILIONI YA RAIS SAMIA

 

Katika kukuza biashara zao Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Burian, amewataka wafanyabiashara ndogondogo kuchangamkia fedha za mkopo wa riba nafuu zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa wananchi.

 

Mkuu wa mkoa ameyasema hayo Disemba 12, 2024 jijini Tanga, wakati akizindua na kugawa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo uliofanyika katika viwanja vya Tangamano mkoani humo.

 

Ugawaji wa vitambulisho hivyo ni mwendelezo wa uzinduzi wa kitaifa uliofanyika jijini Arusha Oktoba 17, 2024 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

 

Balozi Dk Batilda amesema vitambulisho hivyo vitawawezesha wafanyabiashara ndogondogo kupata fursa ya mikopo katika benki ya NMB ambapo Serikali, kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imetenga fedha hizo na zinatolewa kwa riba ya asilimia saba.

 

Amesisitiza kuwa Rais Samia ametoa jumla ya Shilingi bilioni 18.5 kwa ajili ya mikopo na kila mwananchi anayo haki ya kuipata muhimu ni kutimiza matakwa ya mkopo huo.

 

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Tanga ina jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 60,253, kati yao, wanaume ni 37,137 na wanawake 23,116 na kwamba, miongoni mwa hao, 2,306 wametambuliwa, kusajiliwa na kati yao, wanawake ni 1,448 na wanaume 858. 

 

Mkoa wa Tanga umepokea vitambulisho 1,151 vilivyotolewa kwa walengwa ili iwe chachu kwa wengine ambao bado hawajalipia Shilingi 20,000 kupitia control namba inayotolewa na mfumo wa GePG.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments