Jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kufufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), zimesaidia kukuza Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Utalii, kwa kutangaza vivutio na kuwawezesha Watalii kufikia vivutio hivyo na kukuza pato la Taifa.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam amesema kuwa, Ndege ya ATCL imefanikiwa kusafirisha abiria 1,109,803, mizigo tani 10,181 na kufanya safari za ndani na nje ya nchi 16,522 katika vituo takribani 12 vya nje ya nchi.
Mafanikio haya yameonekana kwa kipindi cha kutoka Januari mpaka Disemba 17, 2024, ambapo ATCL ina usalama na utendaji na ina vibali vya usalama wa kufanya safari.
Kampuni ya Ndege (ATCL) imeendelea kufanya vizuri katika biashara ya usafiri wa anga kwa kusafirisha abiria na mizigo ndani na nje ya nchi, hatua ambayo imeinua uchumi na kuiunganisha Tanzania na mataifa mengine.
Aidha, uwepo wa Ndege za kisasa 15 (Abiria 14 na mizigo1) zilizonunuliwa na
Serikali ya Rais Samia, imekua kichocheo katika kuboresha na kuimarisha Sekta ya usafiri wa Anga Tanzania.
Katika kuendesha shughuli zake, ATCL imeendelea kushirikiana na Wataalamu wa ndani na nje ya nchi ikiwemo Kampuni za Kuunda Ndege (Boeing na Airbus) ambao wamekuwa wakisaidia kutoa mafunzo na kufanya mapitio ya uendeshaji wa shughuli zake kwa kuzingatia taratibu za usalama.
ATCL imeendelea kufanya mashirikiano na Mashirika makubwa ya Ndege ikiwemo Emirate Airlines, Ethiopian Airline, Air India, Qatar Airways, APG Airline, Hahn Air, Oman Air, Rwanda Air, Egypt Air,
Proflight Zambia, LAM - Mozambique Airlines, na Fly Dubai.
Mpaka sasa kampuni ya ndege Tanzania ina jumla ya Ndege 18 ambazo ni Boeing 767 – 300F (Mizigo) 1, Boeing 737 – 9 Max 2, Boeing 787 – 8 (Dreamliner) 3, Airbus 220 – 300 4, DE Havilland Q400 5.
Ndege hizi zinafanya safari katika vituo 27, ambapo 15 ni vituo vya ndani ya
nchi (Mikoa) pia vituo vya nje ya nchi ikiwemo (Africa (9), Nje ya Afrika (3) -
Dubai, Mumbai na Guangzhou)
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments