WAZAZI ENDIAMTU WATOA ZAWADI YA CHRISTMAS KWA WATOTO WENYE UHITAJI

 

JUMUIYA ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Endiamtu Wiilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, wametoa zawadi ya sikukuu ya Christmas zikiwemo nguo na vyakula kwenye kituo cha watoto yatima na wenye uhitaji maalum cha Light In Africa kilichopo mji mdogo wa Mirerani.

 

Mwenyekiti wa wazazi kata ya Endiamtu, Ernest Lucumay akizungumza wakati wakikabidhi msaada huo amesema lengo ni kuhakikisha watoto hao wanasherehekea sikukuu ya Christmas kwa furaha.

 

"Hatufahamu mwishilio wetu hivyo ni vyema kuwakumbuka wahitaji kwa kutoa msaada pale tunapoweza ili kuwapa furaha watoto hawa," amesema Lucumay.

 

Katibu wa wazazi kata ya Endiamtu, Agrippina Paulo amesema wametoa msaada kwa watoto hao ikiwemo nguo, mafuta ya kujipaka, mafuta ya kupikia, mchele na unga.

 

"Tumejitoa viongozi na wana jumuiya ya wazazi kupitia matawi na kata na wadau wengine tumeona tutoe msaada huu kwa watoto wa kituo hiki cha Light In Africa," amesema.

 

Mwenyekiti wa CCM Tawi la Zaire, Jema Lilama amesema wanawake wanaowasidia watoto hao wanapaswa kupongezwa na kuombewa kwa Mungu.

 

"Hata huyu mama mkurugenzi wa Light In Africa ni mtu mwema mwenye kuwajali watoto kwani amejitoa mno katika kuwasaidia yatima na wenye uhitaji," amesema Lilama.

 

Mmoja kati ya wasaidizi wa kituo hicho, Mariam Mbwambo akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, amewashukuru waliotoa msaada huo kwa watoto hao.

 

"Tunawashukuru kwa wote mliojitoa kwa ajili ya kuwasaidia watoto hawa ambao kwa namna moja au nyingine watasherehekea vyema sikukuu hiyo," amesema Mbwambo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu-Mirerani

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments