SERIKALI YASISITIZA AMBULANCE TARIME KUTUMIKA KWA MANUFAA YA WANANCHI

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeendelea kuboresha Sekta ya Afya na kuwajali wananchi wake, baada ya kukabidhi gari la huduma za dharura (Ambulance) katika Kituo cha Afya cha Magoto Wilayani Tarime Mkoa wa Mara ambapo imesisitiza gari hilo kutumika vizuri bila ubaguzi.

 

 

Akikabidhi gari hilo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele amesema, gari hilo limelotolewa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia na kuwataka kutumia gari hilo kwa uangalifu bila ubaguzi, na kwamba kutolewa kwa gari hilo kutasaidia kuondoa kero kwa wananchi wa kata hiyo na kata za jirani wanaopata changamoto ya usafiri pindi wagonjwa wanapopewa Rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

 

"Namshukuru Rais Samia kwa namna anavyoboresha Sekta ya Afya, niwaombe wasimamizi wale ambao tunaenda kusimamia gari tukatende haki, kusiwepo usumbufu wala ubaguzi wa mwananchi yeyote katika kupata huduma, " amesema DC Edward.

 

Amewataka wasimamizi wa gari hilo kuhakikisha linatoa huduma ya afya na sio kufanya shughuli zingine na kusema kuwa gari hilo ni la wananchi sio la biashara lipo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

 

"Gari hili sio la biashara kama gharama zitakuwepo mganga atatoa utaratibu na zitakuwa gharama ndogo za huduma na sio biashara, Rais amekuwa akifanya kazi kubwa kuleta vifaa tiba.

 

" Rais anachapa kazi tukisema tuelezee kila kitu tunaweza tusimalize hadi kesho tuendelee kumuombea Rais Dkt. Samia, " amesema Meja Edward.

 

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba, Eliakimu Maswi, amewataka Wananchi wa Tarime Mkoani Mara, kudumisha mshikamano na utulivu wa kisiasa badala ya kukaa na kutafutana na hivyo kuchelewesha maendeleo yao.

 

“Maendeleo ya Tarime yanapaswa kuwa ni jukumu la kila mwananchi, hivyo  viongozi wa siasa mnapaswa kushirikiana badala ya kutafutana, hali hii inachelewesha maendeleo ya hapa Tarime,” amesisitiza Maswi.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments