Wakala ya Barabara Nchini (TANRODS) Mkoa wa Mtwara imeombwa kuweka wazi bajeti maalum ya wajibu wa kampuni kurudisha sehemu ya faida kwa jamii (CSR) kwa ajili ya utekelezaji kwenye halmashauri ili kupunguza halmashauri kuomba miradi ya pesa nyingi zaidi ikilinganishwa na bajeti zilizotengwa.
Hayo yameelezwa leo disemba 20 ,2024 na baadhi ya wajumbe walioshiriki katika kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara kwa mwaka wa fedha wa 2024-2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania Mkoani Mtwara
“Baadhi ya hamashauri zilibainisha vipaumbele vyao vya miradi yao ambayo ilitakiwa itekelezwe kupitia CSR ya mradi mkubwa wa barabara ya uchumi lakini mwisho wa siku bajeti iliyotolewa na halmashauri hizo ni kubwa ukilinganisha na bajeti ya TANRODS” amesema Baisa Abdallah Baisa Mjumbe wa kikao hicho, akizungumzia ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Newala-Masasi.
Akijibia hoja hiyo Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mtwara, Dotto John, amesema kuwa swala hilo amelipokea na atalifikisha makao makuu kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi
Aidha licha ya kutolewa hoja hizo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewapongeza Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini TARURA na Wakala ya Barabara nchini TANROADS kwa kuendelea kuboresha barabara ndani ya Mkoa wa Mtwara na kuongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi.
#KhomeinTvUpdates
✍️Ramla Masali-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments