UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA |WATANZANIA 30,000 KUAJIRIWA

 

Serikali inaendeleza harakati za kuwaletea maendeleo wananchi wake, ambapo sasa inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Bandari ya uvuvi wilayani Kilwa, mkoani Lindi, ambao utapunguza changamoto za ajira kwa vijana.

 

Bandari hiyo ambayo ujenzi wake umeshaanza imeshaajiri vijana 500 wa Kitanzania na ikikamilika itaajiri zaidi ya Watanzania 30,000.

 

Kimsingi bandari hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na kati.

 

Itatoa ajira kwa zaidi ya watu 30,000 na sasa tayari zaidi ya vijana 500 wa Kitanzania wamepata ajira katika hatua za ujenzi.

 

Bandari hiyo itakuwa na eneo la minada ya kimataifa ya samaki na mazao ya bahari na itakuwa na viwanda vidogo vya kuchakata samaki

 

Aidha Meli kubwa za uvuvi za aina zote zitaweka nanga.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments