SERIKALI YA RAIS SAMIA YATAKA MALALAMIKO YA WANANCHI KUFANYIWA KAZI HARAKA

 

Mabadiliko ya kiuongozi yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi yameanza kuleta mabadiliko, ambapo sasa kipaumbele kimetolewa katika kusikiliza kero za wananchi.

 

Katika kulifanikisha hilo Disemba 12,2024 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa akiwa katika ofisi za wizara hiyo, jijini Dodoma, ameiagiza Menejimenti ya Wizara kusimamia Kitengo kinachoshughulikia malalamiko yanayotolewa kwa Wizara, Taasisi na vyombo vya usalama na kuhakikisha wanayafanyia kazi na kutoa mrejesho wa utatuzi wa malalamiko kwa Wananchi.

 

Bashungwa amevitaka vitengo vya Mawasiliano na Habari vya Wizara, vyombo vya usalama na Taasisi zote kuboresha mfumo wa Mawasiliano na habari kwa umma.

 

Katika mazungumzo yake na Wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara amesema ni haki ya Watanzania kupata  taarifa sahihi kwa wakati.

 

“Kuna Malalamiko mengine yanakuwepo kwa sababu hamna taarifa sahihi au taarifa imechelewa, kwa hiyo lazima mhakikishe mnashughulikia Malalamiko na kutoa mrejesho”, ameeleza Bashungwa. 

 

Vilevile, Bashungwa ametoa wito kwa Watumishi wa Wizara kutoa ushirikiano kwake na viongozi wengine wote ili kwa pamoja kutimiza adhima ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwahudumia Wananchi.

 

Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amemkaribisha Waziri Bashungwa na kumhakikishia ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa majukumu katika Wizara hiyo.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments