WATAKAOBAINIKA KUCHELEWESHA UJENZI JENGO LA WAZAZI UKEREWE KUKIONA

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kumpeleka Mkaguzi wa ndani wa Mkoa kukagua mwenendo wa utekelezaji wa ujenzi wa Jengo la wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe kabla hajachukua hatua kwa wazembe watakaobainika.

 

Hatua hiyo imekuja kufuatia Serikali, kuwataka Watumushi wa Serikali kusimamia Sekta ya Afya, kutokana na jitihada za Rais kuwekeza nguvu nyingi katika kuboresha mazingira katika Sekta hiyo muhimu.

 

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, mapema Ijumaa 27 Disemba, 2024 alipotembelea Hospitalini hapo, kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wazazi na kubaini kuna ucheleweshaji wa miezi sita, kinyume na mkataba na kuagiza , ujenzi huo ukamilike ndani ya siku 20.

 

“Serikali imeleta Milioni 900 kwenye Hospitali hii kwa ajili ya kujenga wodi muhimu ya wazazi ili kuboresha huduma bora za afya kwa Wananchi na kuboresha hali ya utoaji huduma hivyo wasimamizi hampaswi kukwamisha juhudi hizi”. Mtanda.

 

Ameongeza kuwa, inashangaza kuona fedha zimeshafika tangu mwezi Machi mwaka huu na walipaswa kukamilisha ujenzi mwezi Juni lakini ni Milioni 700 pekee zimelipwa kwa mafundi ikiwa ni asilimia 85 ya fedha zote na kusababisha kuchelewesha ujenzi huo.

 

Aidha, ameelekeza mzabuni wa milango kwenye Hospitali hiyo ahakikishe anakabidhi mara moja ili iweze kuwekwa na kukamilisha ujenzi na kuhusu majengo  yaliyoandaliwa kufanya upanuzi, ameahidi kuwasiliana na Wizara ili kuhakikisha fedha zinaletwa kukamilisha ujenzi.

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments