CRDB YAKABIDHI CHETI KUTAMBUA MCHANGO WA MADIWANI MBEYA

 





Halmashauri ya Jiji la Mbeya imepokea cheti cha heshima kutoka kwa Benki ya CRDB kwa kutambua mchango mkubwa wa madiwani kwa mashirikiano ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo inayoelekezwa na serikali.

 

Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Mbeya mjini , Jeremiah Msemo amekabidhi cheti hicho leo Alhamisi Januari 30,2025  kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa mara baada ya kushiriki kikao cha Baraza la Madiwani.

 

Amesema cheti hicho mahususi kwa kutambua mchango mkubwa wa baraza la madiwani kwa kushirikiana na benki hiyo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayoelekezwa na serikali ya awamu ya sita.

 

"Tunatoa shukrani kwa madiwani kwa kazi nzuri ya mashirikiano katika kuchangiza maendeleo ya wananchi wetu ikiwa ni malengo ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan,"amesema.

 

Jeremiah amewataka Madiwani  halmashauri ya Jiji la Mbeya kuendelea kushirikiana na benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita kuleta chachu ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

 

Wakati huo huo amehamasisha wananchi Mkoa wa Mbeya kujiunga na benki hiyo ili kuleta matokeo mazuri katika ukuaji wa shughuli za kiuchumi .

 

Kwa upande wake Mstahiki Meya Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa ameshukuru benki ya CRDB kwa kutambua mchango wa baraza la Madiwani na kuwataka kuendeleza mashirikiano hayo .

 

Katika hatua nyingine Issa amewataka Madiwani Jiji la Mbeya kushikamana na kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo haijakamilika katika kata 36 za jijini hapa.

 

"Kwa bajeti yetu ya mwaka wa fedha 2025/26 tunakwenda kukamilisha miradi yote ambayo haijamilika katika kila kata katika nyanja mbalimbali hususani ofisi za serikali za mitaa,"amesema Issa.

 

Amewakumbusha Madiwani kuwa kwa sasa wanaelekea katika uchaguzi Mkuu Oktoba 2025  hivyo wakawe chachu ya kueleza wananchi mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan .

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments