Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya siasa, ulinzi na usalama ya Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kusafiri kuelekea Harare nchini Zimbabwe Januari 31, 2025 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Mhe Rais Samia akiwa nchini Zimbabwe atashiriki mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC ulioitishwa kwa ajili ya kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao utaongozwa na Mhe. Emmerson Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbawe na Mwenyekiti wa SADC.
Aidha Mkutano huo unafanyika kufuatia mkutano wa dharura wa utatu wa wakuu wa nchi na serikali wa Asasi ya siasa na usalama (SADC organ Troika) nchi zinazochangia askari katika misheni ya SADC nchini DRC (SAMIDRC) uliofanyika tarehe 28 Januari 2025 ukiongozwa na Mwenyekiti wa Asasi hiyo Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments