MAPOKEZI YA RAIS SAMIA MAKAMBAKO YADHIHIRISHA MWITIKIO WA USHINDI USIO NA KIFANI

 

Hii ni ishara ya upendo wa kweli haswaa, ambao wameuonyesha maelfu ya wananchi wa Makambako mkoani Njombe, baada ya kujitokeza kwa wingi pembezoni mwa eneo la soko kuu wakiwa katika hali ya shangwe na nderemo kumlaki Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻Septemba 06, 2025.

 


Kutokana na kuridhishwa na sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) sambamba na utendaji wa Mgombea wa nafasi hiyo ya Urais Dkt. Samia, Wananchi hao wamemuahidi kumpa kura nyingi ifikapo Oktoba 29 kwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu.

 

Sambamba na hilo, wameendelea kummwagia upendo kwa kumzawadia wimbo maalumu wenye mashahiri ya kumtakia heri na afya njema nyakati zote katika kuzunguka kwake nchi nzima kunadi sera za CCM na kuomba kura.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments