JIJI LA MBEYA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 22 MAPATO YA NDANI

 

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imejipanga kukusanya zaidi ya Sh 22 bilioni kwa mwaka 2025/26 kupitia vyanzo mbalimbali  vya mapato ya ndani.

 

Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Mohammed Aziz amesema leo Alhamisi Januari 23,2025 kwenye kikao maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Mbeya (DCC) cha kupitia  bajeti ya halmashauri ya Jiji.

 

Aziz ametoa kauli hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa na kwamba  wamejipanga kuongeza  ufanisi na  ubunifu wa vyanzo vya mapato kwa kutumia mashine za poss kwenye maeneo ya masoko ,vituo vya mabasi  .

 


"Katika  makusanyo  hayo  asilimia 70 zitaelekezwa kwenye  mikopo ya asilimia 10 ya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu sambamba na kutekeleza miradi ya maendeleo ya  sekta ya elimu, afya na nyinginezo,"amesema.

 

Amesema lengo ni  kuiwezesha halmashauri  kuongeza wigo wa  kujitegemea kwa asilimia 21  kupitia mapato ya ndani na  kufikia malengo yaliyo kusudiwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

 

Amesema ili kufikia malengo  wameweka mikakati madhubuti ya kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha na ubadhirifu wa miradi ya maendeleo.

 

"Lengo ni kuleta maendeleo ya pamoja sambamba na kudhibiti mianya ya rushwa katika ukusanyaji wa mapato kwa kuelekeza nguvu katika matumizi ya mashine za poss katika  kila kata na kuibua vyanzo vipya vya mapato ,"amesema.

 

Aziz amesema ili kufikia malengo ya kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri kutoka Sh 19 bilioni kwa mwaka 2023/24 mpaka  Sh 20 bilioni  ni kuongeza wigo wa   kushirikisha wadau hususani wa vyama kwa kutoa ushauri na  kuibua  vyanzo vipya vya mapato.

 

 Kaimu Mchumi wa Jiji la Mbeya ,Cosmass Kyovecho amesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 ,halmashauri ilikusudia  kukusanya zaidi ya Sh  87.9  bilioni  mpaka kufikia June 2024 ilikusanya  zaidi ya Sh 93.7 Bilioni sawa na asilimia 107. 

 

Amesema kwa mwaka 2024/25 walikusudia kukusanya kiasi cha Sh 97.5  bilioni na  mpaka kufikia Desemba mwaka jana walikusanya zaidi ya Sh   52.9 bilioni huku kukiwa na mikakati zaidi ya kutanua wigo wa kuongeza  vyanzo vipya vya mapato.

 

Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dourmohamed Issa amesema kuwa bajeti yao imejikita kuhudumia wananchi katika kuleta maendeleo

 

"Mbeya hatuijengi peke yetu hivyo tunaomba washiriki kutoa maono yenu katika bajeti ili kuleta chachu ya maendeleo katika Jiji letu,"amesema.

 

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️ Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments