Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeridhia ufanyaji wa biashara saa 24 katika Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamedhihirishwa na Mkuu wa Wilaya Ubungo Hassan Bomboko Januari 22, 2025 alipokuwa katika majukumu ya kikazi wilayani humo.
"Shughuli za Uzalishaji, Ujenzi wa Taifa kupitia Miradi ya Maendeleo na Biashara zitakuwa zinafanyika Usiku na Mchana,
Bomboko ameongeza kuwa, "Kwakua Stendi kuu ya Mabasi Iko Ubungo- Mabasi yanafanya kazi ya Usafirishaji kwa massa 24 na kwa kutambua Ubungo ndio lango la Jiji la Dar Es Salaam sisi kama Serikali tumekubaliana kuhakikisha shughuli za uzalishaji, ujenzi wa Taifa kupitia miradi ya maendeleo na biashara zitakuwa zinafanyika usiku na mchana" Bomboko.
Aidha, amesisitiza kuwa serikali imejianda na kujipanga kuendelea kuimarisha usalama na amani katika kila eneo la Wilaya hiyo.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments