Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) inatarajia kutoa bure huduma za uchunguzi wa magonjwa ya saratani ikiwemo tezi dume, shingo ya kizazi, matiti na mfumo wa chakula.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Januari 30, 2025 Daktari Bingwa wa Saratani Dkt. Tibera Rugumbwa amesema huduma hizo zitatolewa Februri 4 mwaka huu ikiwa ni siku ya maadhimisho ya saratani duniani.
Amesema lengo la kutoa huduma bure ni kusaidia wananchi kufanyiwa vipimo vya uchunguzi ili kubaini kama wana saratani wapatiwe matibabu.
"Kwa Tanzania kati ya watu 45,000 wakifanyiawa uchunguzi nusu yake hupoteza maisha kutokana na tatizo la saratani kwa wanawake na wanaume ,"amesema.
Ametaja saratani zinazo sababisha vifo kwa mgonjwa akichelewa kupata matibabu ni pamoja na tezi dume, saratani ya shingo ya kizazi, matiti na mfumo wa chakula ambazo hugundulika haraka.
Jesca John ameomba elimu zaidi kuendelea kutolewa kufuatia idadi kubwa kujifungia majumbani kutumia tiba za asili.
✍️ Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments