Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara imebaini mapungufu katika miradi nane yenye thamani ya shilingi 253,300,000.00 kati ya miradi 28 ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Miundombinu pamoja na Afya.
Hayo yamesemwa leo january 31/2025 na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Mtwara Elisante Mashauri ,wakati anazungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TAKUKURU ambapo amesema kuwa wamefungua kesi 9 ambazo zinaendelea Mahakamani, ambapo katika kesi hizo, jamhuri imeshinda kesi Moja.
“katika kipindi cha Januari hadi Machi tutaendelea kuhakikisha kwamba tunazuai vitendo vya rushwa na ubadhirifu katika makusanyo ya mapato kwenye halmashauri ,tutakagua miradi ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa thamani ya fedha inapatikana.”amesema Mashauri.
Aidha Mashauri ametoa wito kwa wananchi na wadau wote kuendelea kushirikiana katika kipindi cha uchaguzi wa viongozi utakaofanyika mwzi Oktoba mwaka huu ili kupata viongozi wasiojihusisha na vitendo vya rushwa kwa maendeleo ya Mtwara na Taifa kwa Ujumla.
"TAKUKURU Mkoa wa Mtwara tunawapongeza na kuwashukuru wananchi pamoja na watu wote Kwa ushirikiano, tunapoelekea katika kipindi cha uchaguzi wa viongozi 2025 tuendelee kushirikiana ili kupata viongozi bora wasiojihusisha na vitendo vya rushwa” amesema Mashauri.
✍️ Ramla Masali-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments