SERIKALI KUPITIA TTCL IMEFANIKISHA UJENZI MKONGO WA MAWASILIANO

 



Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imefanikisha kazi ya ujenzi wa Mikongo ya Mawasiliano ambapo pongezi zaidi zimeelekezwa kwa  Shirika la Mawasiliano la Tanzania (TTCL) na Wataalamu wa ndani kwa kazi kubwa waliyofanya, na kutangaza kuwa kazi hii imekamilika.

 

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa, wakati akikagua Mradi wa Ufikishaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Mombasa, kupitia Kituo cha Horohoro Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga.

 

“Kuanzia mwezi wa pili, mkongo utaanza kutumika na tutatengeneza utaratibu mzuri wa kuja kuzindua na wenzetu wa Kenya ili Watanzania wafahamu na wananchi wa nchi zote zinazotuzunguka wajue kwamba sasa njia hii ya Mkongo kwenda Mombasa imekamilika," amesema Waziri Silaa.

 

“Na wote mnafahamu hawa vijana wetu (Gen-Z), afya ipo katika mawasiliano, habari ipo kwenye mawasiliano, biashara ipo kwenye mawasiliano, elimu ipo kwenye mawasiliano, kilimo kipo kwenye mawasiliano, sisi kama Sekta ya Mawasiliano, kazi yetu ni kuhakikisha maeneo haya yanawezeshwa katika huduma hii ili kuhakikisha TEHAMA inachangia ukuaji wa uchumi wa nchi hii,” amesema.

 

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la TTCL Mhandisi Cecil Francis amesema manufaa ya maunganisho ya Mradi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutoka Horohoro hadi Mombasa ni pamoja na kuimarika kwa maunganisho ya Kikanda, na kuongeza thamani ya mkongo wa Taifa wa mawasiliano na hivyo kufungua fursa mpya za biashara na mapato.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments