SERIKALI, WADAU WAKABIDHI VIFAA KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

 



Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeiongoza Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation, kupitia ufadhili wa Global Fund chini ya Wizara ya Afya, kutekeleza Mpango Jumuishi wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii kwa kununua na kukabidhi vifaa vyenye thamani ya Shilingi 522,032,431, kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii zaidi ya 1,500 katika Mikoa ya Kagera, Tabora, Mbeya na Geita.

 

Zoezi hilo limeongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe ambapo ugawaji wa vifaa hivyo umeanzia Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera Januari 24, 2025, na unatarajiwa kuendelea mikoa mingine, ambapo Serikali na wadau wanaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayosaidia wahudumu hao wa Afya ngazi ya jamii kuwa tayari kwa kuilinda nchi na kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na Afya Bora.

 


"Ujio wa vifaa hivi utachangia, kuongeza hamasa miongoni mwa wahudumu wa ngazi ya jamii, hivyo tukifanya kazi vizuri kupitia vitendea kazi hivi tunavyovipokea kutoka BMF, Tanzania, itakuwa salama, kwasababu mtakuwa mnalinda, hakuna tutakachowapa kinachoendana na kazi yenu ila chochote tutakachowapa kipokeeni kama moyo wa shukrani,” amesema Dkt. Magembe.

 

Akizungumza  kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamini Mkapa Foundation,  Bw. Erick Msunyaro amesema, BMF inaunga mkono jitihada na juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika utekelezaji mpango wa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii, na kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo  Global Fund na Irish Aid  katika awamu ya kwanza  jumla ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii 1,943 wanapatiwa mafunzo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kusomesha wahudumu wa afya ngazi ya jamii 4,747 kwa awamu tofauti," amesema. 

 

“Sisi Benjamin William Mkapa Foundation tutaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha huduma za afya kwa jamii zinaboreshwa, hususan kwa makundi yaliyo pembezoni na yenye uhitaji mkubwa zaidi, lengo letu ni kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama,” amesema Bw. Mnyasuro.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na fulana mbili, mwamvuli, kizibao, buti, begi la mgongoni, kipima joto, koti na koti la mvua kwa kila mmoja.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments