Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewapongeza Wataalam katika Kituo cha Afya Kabyaile, Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera, kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuchunguza sampuli mbalimbali za magonjwa hatarishi ikiwemo yale ya mlipuko.
Pongezi hizo zimetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe Januari 25, 2025 wakati alipoongoza timu ya Wataalam pamoja na Wadau wa Sekta ya Afya, kutembelea na kuona shughuli zinazofanywa katika Maabara tembezi ya Afya ya Jamii iliyopo katika Kituo cha Afya Kabyaile, Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera.
Dkt. Magembe amesema kuwa, ushirikiano zaidi baina ya Serikali pamoja na wadau unahitajika zaidi katika maabara tembezi nchini ili wataalam hao waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa taarifa sahihi za kimaabara kuhusu magonjwa mbalimbali.
Maabara hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika uchunguzi wa sampuli mbalimbali za magonjwa ya mlipuko ambapo imefanya kazi kwa ufanisi kuchunguza sampuli za ugonjwa wa Marburg uliotokea mwaka 2023 pamoja na 2025.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments