SERIKALI YA RAIS SAMIA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUJISAJILI KWENYE MFUMO

 

Serikali kupitia Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo, Hawa Ghasia, imesema kuwa kuanzia Januari 31, 2025, majina ya wafanyabiashara 1,520 waliokuwepo soko la Kariakoo kabla ya ajali ya moto ya Julai 10, 2021, yatatangazwa ili wajisajili katika mfumo wa TAUSI.

 

Mwenyekiti Ghasia amesema taarifa rasmi itatolewa mara baada ya kukamilika kwa upangaji wa kundi la kwanza la waliokuwapo awali.

 

Aidha, amebainisha kuwa hakuna mfanyabiashara atakayerudi sokoni kabla ya kulipa deni lake la awali kwa kuwa kuna wafanyabiashara 366 wanadaiwa zaidi ya sh. milioni 358 kabla ya ajali ya moto, hivyo wanapaswa kulipa madeni yao kabla ya kupatiwa funguo za kurejea sokoni.

 

Soko la Kariakoo lilisitisha shughuli zake mwaka 2021 baada ya kuungua moto, na sasa serikali imekarabati na kujenga jengo jipya kwa gharama ya Sh.Bilioni 28.03 na biashara zitarejea rasmi Februari mwaka huu.

 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametangaza kuwa kuanzia Februari 22, 2025, biashara katika soko hilo zitaendeshwa kwa saa 24.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments