SERIKALI YADHAMIRIA KULINDA MAKABILA YA ASILI NA MAKUNDI MAALUM

 



OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imefanya kikao kazi cha kuwajengea uwezo wasimamizi na watekelezaji wa mpango wa kuwasaidia watu wa makundi maalum na makabila ya asili yaliyo katika hatari ya kutoweka (Vulnerable group).

 

Kikao kazi hicho kimefanyika hivi karibuni katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe Mkoani Morogoro na kimehusisha Waratibu wa mpango wa shule salama, Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Ustawi wa Jamii wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

 

Mratibu wa Shule Salama, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Hilda Mgomapayo ameeleza kuwa kikao hicho ni cha kutathmini hali ya utekelezaji kufuatia ziara iliyofanyika ya  kuwatembelea makundi maalum na makabila ya watu wa asili kwenye mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Arusha na Simiyu.

 

Amesema pamoja na ziara hiyo Maofisa hao walijengewa uwezo  jinsi ya  kuandaa mpango mkakati wa kusaidia makundi maalumu na makabila ya asili.

 

Mratibu huyo ametoa wito kwa wataalamu kushughulikia na kufuatilia kwa haraka changamoto na malalamiko kuhusiana na makundi maalumu yanapojitokeza. 

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments