Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaikusanya Afrika jijini Dar es Salam inapopokea Marais na Wakuu wa nchi zaidi ya 25 za Afrika wanaohudhuria Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika.
Baadhi ya viongozi wanaohudhuria mkutano huo unaofanyika Januari 27 na 28, mwaka huu wameanza kuwasili nchini na kupokelewa na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Viongozi hao walioanza kuingia nchini Januari 25,2025 ni pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina na Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone Julius Maada Bio aliyepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo, tayari kwa kuhudhuria mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNCC).
Wachambuzi wa masuala ya uchumi wameeleza kuwa hii ni hatua nzuri kwa Afrika hususani Tanzania kwani historia imejirudia.
Itakukumbukwa kuwa Tanzania ndio nchi pekee iliyothubutu kuchelewesha uhuru wake kusubiri nchi nyingine za Afrika sanjari na kusaidia nchi nyingi kujikomboa toka kwenye makucha ya wakoloni enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania.
Hili limejidhihirisha tena kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na dhamira yake ya dhati ya kumkomboa mwanamke wa Kiafrika dhidi ya matumizi ya Nishati chafu ya kupikia.
Aidha mkutano huo uliopewa jina la 'Mission 300 - M300' unalenga kuhamasisha upatikanaji wa umeme kwa Waafrika Milioni tatu wa maeneo ya mijini na Vijijini ifikapo mwaka 2030 hivyo mjadala Mkuu unatarajiwa kuwa juu ya njia za kutatua changamoto zinazokwaza upatikanaji wa Nishati hiyo barani Afrika.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments