WAGENI MKUTANO WA NISHATI KUTUMIA BARABARA ZA MWENDOKASI

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetangaza kuwapunguzia adha ya foleni barabarani Wananchi wake, wakati wa mkutano wa Viongozi wa Afrika unaoarajiwa kuanza Januari 27, 2025, kwa Wageni wanaowasili nchini, kutumia njia ya Mwendokasi kwenda na kurudi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. 

 

Akiongea jioni ya Januari 25, 2025, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema kuwa, abiria wanaokwenda na kurudi kutoka mjini wataendelea kutumia barabara ya kawaida na kwamba, nchi yetu imepata bahati ya ugeni mkubwa kuanzia tarehe hiyo, kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Afrika wa Masuala ya Nishati.

 

“Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ametupa heshima kubwa kama Taifa kuleta Viongozi wa Afrika na Dunia kuja kwetu,” amesema Ulega.

 

Aidha, Waziri Ulega  amekagua maandalizi ya miundombinu ya mkutano huo, ikiwemo kufungwa kwa taa za mwanga barabarani ambazo zimeanza kubadili mwonekano wa Jiji la Dar es Salaam nyakati za usiku. 

 

Mkutano wa Nishati wa Bara la Afrika utakutanisha Viongozi Wakuu wa Afrika kujadili namna ya kuongeza upatikanaji wa umeme kwa Wananchi wa Afrika na utafanyika kati ya Januari 27 na 28 mwaka huu.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments