TUZO ZA MLIPA KODI BORA SASA KUITWA ‘TUZO ZA RAIS’

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuanzia mwaka mpya ujao wa kodi (2024/2025), tuzo za Walipa Kodi Bora wa Mwaka zinazotolewa la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zitakuwa zikiitwa “Tuzo za Rais.”

 

Rais Dkt. Samia amezungumza hayo leo Januari 23, 2025 katika hafla ya utoaji tuzo za Mlipa Kodi bora kwa mwaka 2023/2024, iliyofanyika ukumbi wa The Super Dome jijini Dar es Salaam.

 


“Zitakuwa tuzo za Rais, na lengo ni kuipa hadhi kubwa siku hii na kuwapa motisha zaidi wafanya biashara wetu nchini.” Amesema Rais Dkt. Samia.

 

Aidha, Rais Samia ameonya tabia ya baadhi ya Wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi kwa kisingizio wamepewa maelekezo ‘Kutoka Juu’ akisema kuwa “Sijawahi kutoa maelekezo ya mtu asilipe kodi, ikitokea kufanya hivyo nitafanya kwa maandishi.” 

 

Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Samia amaekabidhiwa Tuzo na TRA kwa kutambua mchango wake katika kutambua Dira na Miongozo ya kusimamia ulipaji kodi kwa hiyari na matumizi sahihi ya kodi kwa maendeleo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️ Juma Mohamed

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments